Jukumu la Muuza Mafuta
1. Kuuza mafuta na oili kwa wateja kwa ufanisi wa hali ya juu na kwa kufuata mwongozo wa mwajiri.
Ujuzi Unaohitajika
1. Wenye elimu ya kidato cha nne na kuendelea.
2. Wenye kuweza kutoa huduma bora kwa wateja.
3. Wenye usimamizi wa hela wa hali ya juu (kuhesabu, kurudisha chenji, n.k.)
4. Wenye nidhamu na utii.
5. Wenye uwezo wa kujifunza kwa haraka.
Hauhitaji kuwa na uzoefu wa kuuza mafuta ama wa kufanya kazi kwenye kituo cha mafuta. Kituo kiko tayari kuwapa kazi watu wenye kuonesha uwezo wa kujifunza kazi na kutoa huduma bora kwa wateja.
Kwa sababu ya mahali kilipo Kituo hiki, Vikindu, Mkuranga , waombaji walio karibu na Vikindu, ama ambao wako tayari kuhamia sehemu iliyo karibu kama wakipata kazi, watapewa kipaumbele.
Mshahara
Nafasi hii italipwa shs 180,000 mpaka 200,000 (mshahara baada ya makato)
Tuma CV yenye namba yako ya simu, pamoja na picha yako kwenda [email removed]
Kituo cha kuuza mafuta kilichopo maeneo ya Vikindu, Mkuranga, kinatafuta wauza mafuta (wanaume na wanawake)