KAMA UNATAKA KUITWA KWENYE INTERVIEW, LAZIMA UFAHAMU SIRI HII

Share and send to your friends !
Kinondoni, Bunju Dar Es Salaam
Details
Description

ZINGATIA. Tazama upande wa mkono wa kulia wa tangazo hili. Utaona alama ya Simu. Fuata maelekezo yaliyoandikwa chini ya alama hiyo.

Tabia yako ndiyo inayokuponza. Unatuma CV hiyo hiyo moja kwenye kila tangazo la kazi unaloomba. Na barua ni hivyo hivyo. Unabadili tarehe, kichwa cha habari na nafasi ya kazi unayoomba. Kisha unatuma barua ile ile kila mahali. Halafu kweli unashangaa kwa nini eti hauitwi kwenye interview?

Ndugu yangu Hebu usijidanganye! Hapa Tanzania, kwa kila tangazo moja la nafasi ya kazi (hasa katika sekta binafsi), waajiri hupokea takribani nyaraka 1000 hivi kutoka kwa wanaotafuta kazi. Katika hali kama hii si ajabu kwamba hakuna muda wa kutosha kuzitazama kwa muda mrefu nyaraka za kila mwombaji. Ni wastani wa sekunde zisizozidi 10 hutumiwa kupitia nyaraka za kila mwombaji. Katika hatua hii maombi mengi hutupiliwa mbali na machache tu ndiyo huendelea kusomwa kwa kina zaidi. Na hata kama zingetazamwa kwa muda mrefu, haibadilishi kitu: ya kwamba nafasi inayogombaniwa ni moja au chache na waombaji ni wengi! Kwa vyovyote vile katika hatua hii wengi wataachwa tu. Suala hapa ni je, wewe utakuwa miongoni mwa hao wachache watakaopenya kwa hatua inayofuata? Kwa bahati mbaya katika hatua hii ni nyaraka zako tu ndizo zinazokuwakilisha. Wewe mwenyewe bado haujaitwa wakati huu. Bila shaka kila mtu anatamani kwamba angewakilishwa na nyaraka ambazo zitampa nafasi ya kuitwa na hatua inayofuata ya usaili au mahojiano.

Ni kwa msingi huu, ili upenye katika hatua hii ni lazima maombi yako ya kazi yawe yamepangiliwa kweli. Yawasilishe fikra pevu, yawaaminishe wachambuzi kwa hoja nzito za kitaalamu na kuoanisha wasifu wako wa kazi nyinginezo ulizowahi kufanya kabla na hii unayoomba sasa. Bila shaka si mchezo.

Lakini Usijali. Msaada Uko Hapa!

Ni kweli kuandika maombi ya kazi kunahitaji “Ubingwa” wa hali ya juu. Lakini, katika ulimwengu huu ubingwa si kuandika maombi ya kazi tu. Unaweza kuwa bingwa katika mambo mengine. Na wewe ni shahidi kwamba wapo watu wengi ambao hata kusoma au kuandika ni shida lakini ni “Mabingwa” kweli katika nyanja zingine. Kwa hiyo hapa jambo la msingi ni hili: katika dunia hii huwezi kuwa bingwa katika kila kitu. Fundi wa magari akiumwa ataenda kwa daktari kutibiwa. Na daktari akiharibikiwa gari ataenda kwa fundi magari. Kila mmoja wao akitaka ajue vyote basi mwishowe ataishia kuwa hajui lolote.

Ndiyo maana sisi kabla hatujakusaidia kukuandikia maombi ya kazi ni lazima tutumie muda wa kutosha kuhojiana na wewe kwanza kupata taarifa zako muhimu na wasifu wako kwa ujumla. Ndipo tutakapoweza kufuma pamoja taarifa hizi katika namna ambayo zitajenga sifa zinazotakiwa na mwajiri wa kazi uliyoilenga wewe.

WALENGWA WA HUDUMA HII NI AKINA NANI?

Kimsingi kila anayetafuta kazi na ambaye angependa kusaidiwa kuandika maombi ni mlengwa wa huduma hii. Unaweza kusema kundi mojawapo ni lile la wale waliohitimu mafunzo mbali (Elimu ya juu ya Vyuo vikuu, Vyuo vya kati, Vyuo vya Ufundi, n.k.). Na kundi lingine ni lile la wengine wote waliosalia.

MUHIMU

Sisi Hatutoi Ajira. Wala hatuwashawishi waajiri ili watoe upendeleo wa ajira kwa watu tunaowaandikia maombi ya kazi. LA HASHA! Tunachokifanya ni kushirikiana na wewe kuandika kitaalamu nyaraka za maombi ya kazi. Lakini wajibu wa mwisho ni wa kwako na wewe mwenyewe ndiye utakayefanya uhariri wa mwisho na kuhakikisha kuwa kila kilichoandikwa ni sahihi.

IN ENGLISH

IF YOU WANT TO BE INVITED FOR A JOB INTERVIEW, YOU MUST KNOW THIS SECRET

NOTE: Look at the right-hand column of this advert. You will see the Phone Sign. Follow instructions written below that sign.

Your bad manners (professionally) are to blame for your misfortune. If you are the type who sends the same CV or Cover letter to whatever jobs you apply for, then STOP witch-hunting! You can’t just tweak here and there and expect the CV/Cover letter you sent to multiple places will work. No way!

For every advertised Job Position especially in the private sector, employers and recruitment agencies receive a minimum of 1000 application documents from candidates across Tanzania (i.e., 500 Resumes/CVs and 500 Cover Letters). No wonder the selection committee spends no more than 10 seconds to scan and decide whether a particular candidate’s application package goes into the “YES” section (meaning will be read later in its entirety) or ends up in a “NO” section (end of story). And while we are still here please note that, at this stage in the recruitment process, you are not physically present. It’s only your application documents that speak on your behalf.
Needless to say, it is everyone’s wish that his/her application package demonstrates an edge above the rest of the received applications.

It is on this basis, every job application material you submit (cover letter, resume/CV, etc.) must be unique in every way: polished, precise, professional, consistent, and balanced to perfection. It needs to go beyond mere chronological order/list of your experience, skills, and employment history. But how is that even possible?

Don’t worry. Help Is Here!

Writing is an art. But, there are many people in this world who are Geniuses in different areas except for writing. The bottom line is; you can’t be good at everything. And let’s face it, your ignorance in other areas of life is what made you dedicate all the time to that single area where they call you “Genius” or they simply agree that you always do what you do best. At Business Consultancy Services, this truth is not just understood but it’s a way of life. That’s why ample time is spent with you to understand your history, skills, experience, strengths, etc., and how all these can be brought together to produce the right mix of information that will sell you to potential employers in the most effective and appropriate way.

WHO ARE THE TARGET BENEFICIARIES?

Generally, every Job Seeker in Tanzania especially FRESH GRADUATES from Universities, Colleges, or other training institutions – VETA, tourism, and hospitality industry, etc.

DISCLAIMER

We are not an Employer or Recruitment Agency. We don’t lobby employers for certain applicants to be employed. We are limited to partnering with the clients/applicants to identify opportunities and collaboratively write Job Application Documents that provide the best chance to be shortlisted for an interview. The client/applicant is solely responsible for final edits, submission to recruitment agency/potential employer, and any claims arising out of or relating to such submission

Apply for this job
Contact via Phone

KISWAHILI

Kuomba msaada siyo udhaifu wala ujinga. Ni ujasiri. Ni kutambua kuwa wewe si bingwa kwenye kila kitu. Bofya alama ya simu hapo JUU. Tutumie ujumbe mfupi wa maneno usemao: KWANI SHILINGI NGAPI? kwenda namba hiyo. Iwe uko Mkoani kijijini, shambani, au mjini, tunaongea kila kitu kwa simu na tunakutumia nyaraka kwa internet. Malipo ni madogo sana. Na ni pale tu utakaporidhika na ubora.

ENGLISH

To seek help is not a weakness. It’s being brave. It’s to understand that you don’t know everything. Click on the Phone Symbol ABOVE. Send a Short Text Message: HOW MUCH? to this number. Whether you are in rural areas or towns we have you covered. We speak on the phone and send documents on the internet. Our rates are affordable and you only pay if satisfied.

You need an account to contact this user. Please
Kinondoni, Mikocheni Dar Es Salaam Details Description We are looking for an ambitious Junior Accountant to provide support to the financial department by managing daily accounting tasks. You will be…