Vacancy title:
5 Tabibu II (Clinical officer)
Jobs at:
Arusha City Council
Deadline of this Job:
18 December 2020
Within Tanzania , Arusha , East Africa
Summary
Date Posted:
Monday, December 14, 2020
, Base Salary:
Not Disclosed
JOB DETAILS:
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji anawatangazia Watanzania wote wenye sifa na nia ya kufanya kazi katika Jiji la Arusha kutuma maombi ya kazi ya muda kwa Mkurugenzi wa Jiji ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya Tangazo hili. Nafasi hizi ni za muda wa miezi sita kwa kazi zilizopangwa na kuidhinishwa na Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2020/2021. .
Kazi na Majukumu
• Kutambua na kutibu magonjwa ya kawaida.
• Kusimamia utendaji wa watumishi walio chini yake na kufanya upasuaji mdogo.
• Kushiriki katika kupanga na kutekeleza Huduma za Afya Msingi.
• Kushauri na kuhamasisha wananchi kuchangia huduma za Afya za Mfuko wa Afya ya Jamii.
• Kuweka kumbukumbu za vifaa na zana za kutolea huduma.
Job Skills: Not Specified
Sifa zinazotakiwa
Awe mhitimu wa kidato cha nne/sita mwenye Stashahada ya Tabibu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Job Education Requirements: Not Specified
Job Experience Requirements: Not Specified
Work Hours: 8
Job application procedure
MAELEZO YA JUMLA
• Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na Mwenye akili timamu.
• Waombaji wawe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
• Barua za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti vya Elimu/taaluma, cheti cha kuzaliwa na maelezo binafsi (CV).
• Mshahara utakuwa wa makubaliano kwa kuzingatia bajeti.
• Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 18/12/2020 saa 9:30 alasiri.
• Maombi yatakayotumwa kwa mkono hayatapokelewa.
• Waombaji wenye uzoefu wa kazi watapewa kipaumbele.
Maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo:
Mkurugenzi,
Halmashauri ya Jiji la Arusha
S.L.P. 3013, Arusha.