NAFASI ZA UTANGAZAJI NA KUENDESHA KIPINDI CHA TAARABU

Other Dodoma District Dodoma
Details
Description

Mtangazaji wa kipindi cha Taarabu:

? Awe mwenye kuufahamu musiki wa taarabu kwa kiasi kikubwa na mwenye kupenda taarabu.

? Awe mwenye kufahamu mahadhi ya taarabu na yanavyofaa kuandaliwa

? Awe mwenye kufahamu utamaduni wa taarabu na namna bora ya kuifanya music pendwa kwa wasikilizaji wake.

Majukumu Ya Msingi:

? Kukusanya na kutoa taarifa mbalimbali katika redio

? Kuandaa na kurusha vipindi vya radio

? Kukusanya na kuripoti kwenye mambo ya msingi yanayotokea kila siku na haswa mkoani Dodoma

? Kuhudhuria vikao vya wito wa waandishi Habari, kufanya mahojiano na kuripotia radioni

? Kufanya programu za mambo au matukio ya kila siku ambazo zinavutia wasikilizaji

? Kutafiti, kujiridhisha, kuzibitisha taarifa muhimu wakati wa kujadili maswala mbalimbali wakati vipindi vikiendelea

? Kutoa ushirikiano kwa watangazaji wengine

? Kufanya majukumu mengineyo

Mwombaji awe sifa zifuatazo:

Awe na Shahada (Degree) ya Uandishi wa Habari/Utangazaji au Stashahada (Diploma) ya Uandishi wa Habari/Utangazaji na hata astashahada (Certificate) ya Uandishi wa

Habari/Utangazaji. Pia, awe mbunifu na mwenye kipaji cha utangazaji.

Namna ya Kuomba:

Mwenye sifa hizo anatakiwa atume CV, Barua ya maombi kupitia email hii: [email removed] (Kichwa cha habari cha email yako kiwe ni nafasi

unayoomba). Kama unahitaji ufafanuzi pale ambapo ujaelewa tangazo hili unaweza kupiga simu kwa Ismael Nassary [mobile number removed]. Fahamu tunahitaji utulivu wa kupokea na kupitia maombi yako na waombaji wengine.

Angalizo: Usiambatanishe vyeti vyako wakati wa kuomba kazi hii bali CV yako iwe na referee ambao ulishafanya nao kazi kama wasimamizi wako.

Muombaji aje na nakala zilizothibitishwa (certified copies) za cheti cha kuzaliwa na vyeti vya taaluma tajwa. Mwisho wa Kuomba: 15/10/2020

Kwa Sababu ya muda na maombi kuwa mengi, tutawapigia wale tuu watakaochaguliwa kufanyiwa uasahili. Mteja wetu ni mwajiri anayejali usawa katika kuajiri wafanyakazi.

Kwa niaba ya mteja wetu aliyepo katika wilaya mojawapo mkoani Dodoma tunapenda kuwatangazia nafasi za kazi ya uandishi wa habari na utangazaji katika vipengele vifuatavyo: 1. Mtangazaji wa kipindi cha taarabu 2. Vipindi vya kuelimisha, Kijamii, Kiuchumi na kisiasa

Apply for this job
Partagez et envoyez cette annonce à vos amis !