Mtendaji wa Kijiji III Job at Maswa District Council – Career Opportunity in Tanzania

Overview
Job Category: Government
Job Type: Full-Time
Deadline of this Job:  17 August 2020
Duty Station:  Dar es Salaam, Tanzania
Posted: 05-08-2020
Requirements
Job Description

Vacancy title:
Mtendaji wa Kijiji III

[ Type: FULL TIME , Industry: Public Administration, and Government , Category: Civil & Government ]

Jobs at:

Maswa District Council

Deadline of this Job:
17 August 2020  

Duty Station:
Within Tanzania , Maswa , East Africa

Summary
Date Posted: Wednesday, August 05, 2020 , Base Salary: Not Disclosed


JOB DETAILS:
Kumb. Na. MDC/CADM/10/1100/61
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imepata kibali cha ajira mbadala chenye Kumb. NA. FA. 170/533/01"A"/119 cha tarehe 29 Juni, 2020 kwa ajili ya kuajiri Watendaji wa Vijiji wawili (2).

Kwa kibali hicho Mkurugenzi Mtendaji (W) Halmashauri ya Maswa anawatangazia Watanzania wote wenye sifa kuomba kujaza nafasi wazi za Watendaji wa Kijiji daraja la III, kuanzia leo tarehe 03/08/2020 .

KAZI/MAJUKUMU YA MTENDAJI WA KIJIJI
• Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
• Kusimamia ulinzi na Usalama wa Raia na mali zao, kuwa mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala bora katika Kijiji.
• Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
• Kuratibu Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
• Kutafasiri na kusimamia sera, Sheria na Taratibu.
• Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na uzalishaji mali.
• Kiongozi wa Wakuu wa vitengo vya kitaalam katika Kijiji.
• Kusimamia kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za kijiji.
• Mwenyekiti wa kikao cha Wataalamu waliopo katika Kijiji.
• Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na mgogoro ya wanananchi
• Kusimamia utungaji wa sheria ndogo za Kijiji.
• Kazi zingine utakayopewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri.


Job Skills: Not Specified


SIFA ZA MWOMBAJI
Mtendaji wa Kijiji III
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV/VI aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/cheti (NTA LEVELS 5) katika moja ya fani zifuatazo:- Utawala, Sheria, Elimu ya Jami (Sociology), usimamizi wa fedha Maendeleo na Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa za Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na serikali


Job Education Requirements: Not Specified


MSHAHARA
Ngazi ya mshahara ni TGS B


Work Hours: 8

 

Job application procedure
MASHARTI YAJUMLA KWA WAOMBAJI
• Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45.
• Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa.
• Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed curriculum vitae) kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (Referees watatu (3)
• Maombi yote yaambatane na picha 2 (passport size) nakala za vyeti vya taaluma, vyeti vya Kidato cha nne na Kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa zilizoelekezwa hapo juu.
• Testimonials provisional Results" Statement of Results" hati matokeo ya kidato cha nne na sita (Form IV & Form VI Results slips) havitakubaliwa/havitafanyiwa kazi.
• Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU, NACTE na NECTA).
• Waombaji waliositaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Mamlaka husika.
• Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 17/08/2020 saa 9:30 alasiri
• Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika Tangazo hili hayatafanyiwa kazi.
• Maombi yote yatumwe kwa anwani hapa: Mkurugenzi Mtendaji (W), Halmashauri ya Wilaya, S.L.P. 170, MASWA
• Tangazo hili linapatikana katika Tovuti ya Halmashauri www.maswadc.go.tz Tovuti ya Secretarieti ya Ajira www.ajira.go.tz   na katika mbao za matangazo za Halmashauri na Mkoa wa Simiyu.


Partagez et envoyez cette annonce à vos amis !