Mpiga Chapa Msaidizi Job at Public Service Recruitment Secretariat – Career Opportunity in Tanzania

Share and send to your friends !
Overview
Job Category: Government
Job Type: Full-Time
Deadline of this Job:  23 February 2021
Duty Station:  Tanzania
Posted: 11-02-2021
Requirements
Job Description

Vacancy title:
Mpiga Chapa Msaidizi

[ Type: FULL TIME , Industry: Public Administration, and Government , Category: Civil & Government ]

Jobs at:

Public Service Recruitment Secretariat

Deadline of this Job:
23 February 2021  

Duty Station:
Within Tanzania , Dar es Salaam , East Africa

Summary
Date Posted: Thursday, February 11, 2021 , Base Salary: Not Disclosed


JOB DETAILS:
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/L/30 09 Februari, 2021
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya ya Lushoto, Ngara, Nzega, na Mpanda anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi kumi na moja(11) kama zilivyoainishwa katika tangazo hili. .

MWAJIRI: KATIBU MKUU, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE.
Mpiga Chapa Msaidizi - (NAFASI 1)
MAJUKUMU YA KAZI
• Kukunja karatasi ngumu na kutengeneza ‘covers’ za vitabu, majarida, madaftari katika mahitaji mbalimbali kwa kugandisha, kuweka pamoja au kushona katika hali mbalimbali za ubora;
• Kukarabati vitabu, kumbukumbu mbalimbali au majarida kwa kuyawekea gamba jipya au kurudisha katika hali yake ya mwanzo kutegemea na kifaa hicho kilichoharibika;
• Kupanga vifaa vilivyotegenezwa katika makasha kwa vipimo vyake au katika seti;
• Kuendesha mashine za kukata karatasi/kupiga chapa/mashine za composing, kushona au kugandisha vitabu, majarada, madaftari na vifaa vingine vinavyokuwa vimetakiwa kwa mtindo na ubora wake; na
• Kupanga karatasi zitakazochapwa kwa hesabu ya kila kitabu, jarida, daftari na vinginevyo kwa kushonwa au kugandishwa pamoja.


Job Skills: Not Specified


SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au VI katika masomo ya sayansi au Sanaa, wenye cheti cha majaribio ya ufundi Daraja la I (Trade Test Grade I) katika “lithography/composing/binding/mashine Minding”, au waliohitimu mafunzo ya miaka miwili ya kupiga chapa.
MSHAHARA: Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B


Job Education Requirements: Not Specified


Job Education Experience: Not Specified


Work Hours: 8

 

Job application procedure
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
• Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45.
• Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
• Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
• Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
• Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
• Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE). • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
• Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
• Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
• Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 23, Februari, 2021.
• Muhimu, kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
S.L.P. 2320 DODOMA.
• Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/   (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
• Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
LIMETOLEWA NA;
KATIBU
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA


POST SUPPLIES ASSISTANT – 1 POST POST CATEGORY(S) PROCUREMENT & LOGISTIC MANAGEMENT EMPLOYER National Housing Corporation(NHC) APPLICATION TIMELINE: 2021-03-04 2021-03-18 JOB SUMMARY NA DUTIES AND RESPONSIBILITIES i. To enter receipts…
Payable Accountant    Role Description Company Description: Sokowatch is transforming communities across Africa by revolutionizing access to essential goods and services. By connecting small shops to the digital economy, we…
Industry: Manufacturing Location: Morogoro Minimum Education: Bachelor Degree Required Experience: At least 5 years of Experience Reports to: Finance Director Level: Managerial Job Purpose To provide product costing and inventory…